Friday, 9 February 2018

RIWAYA YA LUSIFA : Sehemu Ya Kwanza



                    Tina ni msichana mrembo aliyekamilika kila idara, uzuri wa sura yake, umbo lake na tabia unamfanya avutie zaidi. Kitu kinachoaminika kuwa ni kasoro kwa Tina, binti huyu hakutokea kwenye familia ya kitajiri. Tina alitokea kwenye familia yenye hali duni sana. Licha ya uzuri wake; Tina alipendelea kushinda mgahawani akimsaidia kazi ndogo ndogo mama yake.

                    Mama Tina ambaye ni mama mchapa kazi anayependa kujishughulisha hakuwa na bahati ya kuolewa lakini katika usichana wake alibahatika kuzaa watoto wawili Tina na kaka yake Frank ambaye inasemekana alienda mjini miaka 10 iliyopita.

                   Baada ya kuishi na mama yake kwa kipindi kirefu kijijini, Tina aliona ni vyema aende mjini kumtafuta kaka yake aliyeitwa Frank.Hili ni wazo tu lililomjia kichwani mwake tu. Katika hali ya uhalisia Frank hakwenda mjini, katika kipindi chote hicho Frank alikuwa falme za kuzimu zilizokuwa zikitawaliwa na shetani mkuu yaani LUSIFA.

                  Jioni moja Tina na mama yake walifunga mgahawa mapema sana hali iliyowapa nafasi kubwa ya maongezi. Tina hakutaka kufanya makosa aliamua kutumia vyema muda huo kumshirikisha mama yake dhamira yake ya kwenda mjini kumtafuta kaka yake Frank. 

"mama" aliita Tina
 "abee mwanangu" aliitika mama Tina
  "kuna jambo nataka kukueleza" aliongea Tina kwa sauti ya upole huku akiangalia chini kwani hakuweza kuona pakuanzia kumlainisha mama yake, kwani alijua fika sio rahisi kukubaliwa.
"Ongea mwanangu mpendwa nakusikiliza" aliongea mama Tina Tina alikosa ujasiri wa kuendelea hivyo alibaki kimya
 "Ongea mwanangu nakusikiliza" alirudia tena mama Tina huku akimshika Tina begani. Hali hiyo kidogo ili mpaka moyo Tina hivyo akaamua kasema,
"mama nataka niende mjini "aliongea Tina
" looh ushaanza, hivi Tina unajiona umekuwa eeh si ndio?" aliuliza mama Tina kwa jazba Hali iliyomtisha sana Tina
 "hapana sio hivyo mama" alikanusha Tina "nataka nikamtafute kaka Frank" aliongeza Tina.
 "Na pale mgahawani nitasaidiwa na nani? Aliuliza mama Tina kwa hasira
  " Kuhusu hilo tu usijali kwani nishaongea na rafiki yangu Anna, hivyo kuanzia kesho asubuhi atakuwa anakuja kukusaidia kwa kipindi chote nitakapokuwa mjini? "alijibu Tina kwa ujasiri
 " Na kuhusu LUSIFA je?" alijikuta akiropoka mama Tina
 "Lusifaa ...!!!!?? Ndo dubwashona gani " aliuliza Tina kwa mshangao.
 " nimedhamiria mama ni lazima nimpate kaka yangu Frank, kesho asubuhi na mapema nitaianza safari yangu" alimalizia Tina na kuingia ndani.

            Mama Tina alipigwa na butwaa kwani alichokitamka hakupaswa kukitamka mbele ya Tina. Roho ikamdunda mama Tina kwa mbali alihisi pepo na ngurumo za kuzimu ,Ghafla hofu ikamjaa, amani ikatoweka moyoni mwake kwani alijua fika sasa Roho ya LUSIFA imeanza kuifuatilia na damu ya mwanaye Tina kama ilivyokuwa kwa kaka yake Frank Licha ya mama Tina kusambaza taarifa za uongo juu ya Kijana wake Frank ingali hali halisi anaijua, Mama Tina hakupenda kabisa bintiye Tina ajue kuwa yeye ni mchawi na moja la masharti aliyopewa na mkuu wa mashetani ambaye LUSIFA ni Tina asije akaujua mji yani azaliwe kijijini, akulie kijijini na afie kijijini, kwani akiujua mji tu Rungu la LUSIFA toka falme za kuzimu litamshukia Mama Tina. Na Mama Tina anausiku mmoja tu wakuepa Rungu hilo toka kuzimu.

 Itaendeleaaaaaaaaaa.............!!!!!!!!!!!! 

Je, Mama Tina Atafanya nini kumzuia Tina asiondoke wakati Tina ameshadhamiria kuondoka usikose LUSIFA SEHEMU YA PILI. TAFADHALISHARE PIA USISAHAU KUACHA MAONI YAKO NI MUHIMU SANA.

No comments:

Post a Comment