Saturday, 10 February 2018

RIWAYA YA LUSIFA : Sehemu Ya Pili


Ilipoishia.......

        Mama Tina hakupenda kabisa bintiye Tina ajue kuwa yeye ni mchawi na moja ya masharti aliyopewa na mkuu wa mashetani ambaye ni LUSIFA, ni Tina asije akaujua mji yani azaliwe kijijini, akulie kijijini na afie kijijini, kwani akiujua mji tu Rungu la LUSIFA toka falme za kuzimu litamshukia Mama Tina. Na mama Tina anausiku mmoja tu wakukwepa Rungu hilo toka kuzimu.

Endelea....

         Mama Tina aliwaza sana juu ya hiyo adhabu ambayo angeweza kupewa endapo Tina ataenda mjini, baada ya muda kidogo wazo likamjia kichwani aende kwa Mzee Rwambe ambaye ni kiongozi wa wachawi wa kijiji hicho kupeleka taarifa hizo,ilikuwa ni majira ya saa mbili za usiku muda huo.

"we Tinaaa" aliita mama Tina
  "abee mama" aliitika Tina
"mimi natoka kidogo, narudi sasa hivi" aliongea mama Tina
  "mmmh unaenda wapi usiku huu?" aliuliza Tina
  "maana siyo kawaida yako" aliongeza Tina
"eeeh makubwa..!!" alishangaa mama Tina
 "wewe mtoto mbona siku hizi unanifuatilia sana, nimeitwa na Mzee Rwambe" alijibu mama Tina Roho ilimdunda sana Tina akainamisha kichwa chini ghafla alijikuta akiropoka
 "wewe mama Mzee Rwambe si ndo yule mzee mchawi?"
 "shiiii iiih, kelele...." mama Tina alimnyamazisha Tina
 "tena shika adabu yako, nije nikusikie; nitakukata masikio;huna adabu" aliongea mama Tina kwa ukali huku akimtazama Tina kwa hasira.
Hali ile ilimtisha sana Tina hivyo hakuwa na lakusema
 "sawa mama nenda" Tina aliongea kwa sauti ya chini.

 Mama Tina akaondoka zake kuelekea kwa Mzee Rwambe. Huku nyuma Tina alibaki akijiuliza maswali mengi sana kwanini leo hii mama anahasira hivi ? Kwani yeye hupendi kumuona mwanae wa kumzaa.. ?!! ikizingatiwa hajamuona kwa kipindi kirefu kiasi hiki. mmmmh na kama ni hivyo kwa nini aitwe na Mzee Rwambe usiku huu? Hivi Anna si aliniambia yule mzee ni mchawi au sio yeye? mmh nisije nikawa namuhisi vibaya bure mzee wa watu ngoja nimalizie kukunja nguo mbili tatu hizi niende nikamuulize Anna vizuri .

    Nusu saa baadae mama Tina alikuwa kashafika nyumbani kwa Mzee Rwambe. Mzee Rwambe alikuwa ni mchawi hasa uchawi wake haukuwa wa chini chini kwani alijiamini sana alikuwa anauwezo wa ajabu hata katika zile falme za kuzimu Mzee Rwambe alikuwa na cheo, nyumba yake ilikuwa na mauza uza mengi sana. Wakati mwingine Rwambe alikuwa anaweza asionekane kijijini hapo hata miezi sita lakini matukio ya kichawi anayowaachia mtatamani awahi kurudi ili yapungue. Hakukuwa na mwanakijiji mwenye uwezo wa kumhoji wala kumuongelesha na kila aliyejaribu kumuongelesha basi alimnyenyekea sana vinginevyo umauti ungeweza kumfika mara moja. Alipo fika mahali hapo mama Tina alianza kugonga mlango ngo ngo ngo

  "Hodi Hodi" aliita mama Tina Lakini hodi yake haikupokelewa
 "Hodi, wenyewe " alirudia kuita tena mama Tina Lakini hali ikawa ni ile ile hakukuwa na mtu wa kuweza kuitikia, akatakata kuita tena kwa mara ya tatu Kikasikika kishindo kizito toka ndani mfano wa gunia la kilo mia la maharagwe likianguka, Mmmmh kuna nini humu ndani? Alijiuliza mama Tina.

      Ikumbukwe Mzee Rwambe hakuwa na mke wala watoto aliokuwa akiishi nao nyumbani pale. Hivyo ilimlazimu mama Tina kuhitaji kuchungulia ili kujua nini kimemkuta Mzee Rwambe pengine amepatwa na tatizo. Basi Mama Tina akasogeza jicho lake taratibu eneo la mlango lenye upenyo litakalomuwezesha kuona nini kinaendelea ndani ya ile nyumba, katika hali ya kustahajabisha mama Tina aliona mtu anayefanana na yeye akichomwa kisu na mtu anayefanana na mwanae Tina huku Mzee Rwambe akimshangilia Tina kwa kitendo hicho cha kishujaa. Upesi akaondoa jicho lake kwenye ule upenyo wa mlango, huku mapigo ya moyo yakimwenda mbao. Mama Tina ambaye pia ni mchawi kwa kutoamini kile alichokiona "mmmh hivi naota?" alijiuliza peke yake kwa sauti ya chini chini.

Hali ikabadilika ghafla pepo zikaanza kuvuma, wingu zito likatanda, radi zikaanza kumulika tetemeko likatawala ardhi ya pale kwenye ile nyumba; Hali hii iliongeza hofu na woga kwa Mama Tina. Lakini mama Tina alipiga moyo konde akafikicha macho yake kisha akalisogeza tena jicho lake taratibu kwa mara nyingine kwenye ule ule upenyo huku akitetemeka, lakini hakuona kilichobadilika aliendelea kuona vile vile. Maskini Mama Tina hakujua cha kufanya mwili ukaanza kumsisimka hofu ikazidi kuongezeka wakati akiendelea kuzubaa na kutoamini macho yake kwa kile anachokiona. " Mama aaaaaaah .....!!!! " mama Tina alipiga kelele

 Itaendeleaa.......... Je , ni kipi kilichomsibu mama Tina? Unadhani ni kwa nini mama Tina alikutana na mauza uza ya namna hii?

Usikose kufuatilia SEHEMU YA TATU LIKE & SHARE BILA KUSAHAU KUCOMMENT MAONI YAKO NI MUHIMU SANA KWANGU USISAHA KUFOLLOW BLOG YETU.Ahsante

No comments:

Post a Comment